Injili ni nini?
Injili ni neno ambalo yawezekana sisi sote tumelisikia mara nyingi katika maisha yetu ya kila siku ya Ukristo wetu. Hata unapomueleza Mkristo mwingine yeyote atakwambia kuwa injili ni “Habari njema”. Na hata unapomueleza Mkristo huyo hizo habari njema anaweza kufikiri vizuri kwa kujiuliza swali Je, ni habari zipi hizo? Na hata akaweza kukupa majibu tofauti tofauti ya kukushangaza sana! Msomi, na Profesa wa Agano Jipya katika chuo theolojia, David Seccombe anaandika akisema “Injili ni muhimu kwa sababu watu wanaishi katika mwili na injili ndiyo inayotupa uzima, na ni pekee inayotupa uzima.” Injili ni muhimu kwa sababu watu wanaishi katika mwili...