×
Editors’ note: 

Swahili translation by Raphael Mukanya (DRC- Congo)

Dunia yetu imejaa na habari za uongo na pia Injili za uongo. Mungu pia anakua na Injili ambao ni Injili ya kweli na ni Injili ya Mungu. Injili ni utangajazi wa kimapinduzi ya kwamba Yesu ni mfalme. Tangazo hili linaimarishwa ndani ya Mungu Mmoja, Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, ambao wanajuana, wanapendana, na kutukuzana. Mungu huyu aliumba vitu vyote vionekanavyo na visivyo onekana, na kwa hiyo anastahili utukufu wote na kuhimidiwa. Mungu huyu amenena kupitia Mwanawe na Neno lililo andikwa kwa Agano la Kale na Agano Jipya.

Mungu huyu huyu ndiye aliyeumba wanadamu, mwanaume na mwanamke. Kwa kusikitisha walimuasi Mungu na kujitenga mbali naye na kupotoshwa kwa kila hali ya uutu wao.

Tangu milele, Mungu aliamua kwa neema kuwaokoa watu mwenyewe kutoka kila kabila, lugha, watu na taifa. Injili ni mpango wa Mungu wa kuokoa watu wake kupitiya Mwanawe, ambaye ni Mwokozi, Bwana na Mfalme.

Mfalme huyu alitarajiwa katika maandiko ya Agano la Kale na alikuja duniani kwa mda na wakati. Huyu Mfalme mshindaji alishinda zambi, kifo na shetani msalabani na katika ufufuko wake. Kupitia kifo chake na ufufuko, alishinda nguvu za ulimwengu na nguvu za kiroho za uovu. Mfalme huyu ndiye yule mpatanishi mmoja kati ya mwanadamu na Mungu ambaye msalabani alijifanya msimamizi wetu kamili na wa mwisho kusudi ya kutuliza hasira ya Mungu; Mfalme asiyekuwa na zambi ambaye alichukuwa gazabu ya zambi zetu na kwa hiyo alipatanisha Mungu na watu wake; Mfalme anayewahesabia watu wake kwa neema tu kupitia imani na si kwa matendo yao.

Mfalme huyu anavamia maisha ya wafuasi wake kupitia Roho Mtakatifu wake, Roho mwenye uwezo ambaye anaokoa wale wanaotubu zambi na kuamini. Mfalme huyu hukusanya wafuasi wake katika jamuiya mpya ili wapate kuwa mashahidi wake katika maneno na matendo. Anachochea na kuhimiza watu wake kwa kuanzisha na kuimarisha ufalme wake ulimwenguni pote kwa kuwa chumvi na mwanga katika kila uwanja wa maisha. Baada ya kupaa mbinguni kwa mwili, Mfalme huyu atarudi kama muhukumu wa mwisho na atashinda na kukamilisha ufalme wake katika mbingu mpya na dunia mpya.

Amenena maneno haya katika Injili na anawaita wanafunzi wake kutangaza Ufalme wake kwa njia hiyo. Mfalme huyu anawaita watu wote kila mahali waweke silaha zao chini katika kujisalimisha na waweze kutubu na kuamini. Je! Umefanya hivyo? Ikiwa sio sasa, basi ni lini?

Click here for a version of this article in English

Click here for a version of this article in Shona

LOAD MORE
Loading